Machapisho Mapya

Latest Post

Blog - The Habari

Je hii ni blog yako, wasiliana nasi kutolea maelezo zaidi.
Kliki hapa kutazama blog hii

Blog - Jiachie Blog

Je hii ni blog yako, wasiliana nasi kuweka taarifa zako zaidi.
Tembelea blog hii hapa

Wanablog wa Tanzania wawe wabunifu wa machapisho yao


Bwana Freddy Chacha (pichani kulia) katika blog yake ya "Makala zangu" amechapisha chapisho la kiuchambuzi juu ya

ubunifu wa machapisho kwa wanablog wa kitanzania badala ya kunakili na kupachika katika blog zao.

Nimepitia chapisho lake mwanzo hadi mwisho na kuridhika na mtazamo alioutoa na kufarijika kuona kuwa kuna wanablog wanaotazama uwanda wa blog na kuchangia katika kuleta maendeleo katika uwanda huu.

Chapisho lake lipo katika lugha ya kiingereza na linaanza kama ifuantavyo;


"The blogging phenomenon kicked off in late 1990s- but in Tanzania was picked up by news reporter Ndesanjo Macha -a decade ago.  As Ndesanjo (pictured below) campaigned tirelessly for Swahili blogging, running workshops and attending world wide conferences while maintaining hold on his Jikomboe blog very few understood the meaning of the word, let alone using the internet as feverishly as today. Those days, Ndesanjo confessed he was blogging for love arguing this was the future of global communication.

Other local bloggers started getting noticed after the vicious murder of a Tanzanian couple  in the USA  September 2006. Suddenly we were dependant on Michuzi and internet Radio Butiama to get information that was not readily available on mainstream media.  I personally began blogging in 2007.
How things have changed since!..."


Kama mdau wa blog Tanzania nakushauri upitie ili kuhamasika juu ya kuandika machapisho ya kipekee katika blog yako, Chapisho hilo linapatikana katika kiungo hiki "CALL FOR TANZANIAN BLOGGERS TO BE ORIGINAL AND INVENTIVE"

Sababu 5 kuu zinazowafanya watu wablog

all tanzania blogs
Kuna sababu nyingi zinazofanya watu waanzishe blog, lakini wengi wanaelezea kuwa wanablogu  kwa
sababu moja au zaidi kati ya sababu tano nitakazozielezea katika chapisho hili. Sababu hizi ndizo sababu kuu zinazowafanya wengi wa wanablog kuanzisha blog. Sababu hizi ni kwa wanablog wengi bila kujalisha aina ya mada anayoizungumzia iwe siasa, biashara, afya, elimu ama hata blog ya picha tu.

Kabla ya kuanzisha blog, tafakari ni sababu ipi inayokufanya utake kuwa mwanablog. Je malengo yako ya muda mrefu na mfupi ya kuwa mwanablog yanaendana na sababu inayokufanya uwe mwanablog? Hakikisha kuwa sababu inayokufanya kuwa mwanablog inaendana na malengo yako kinyume na hapo kuna uwezekano mkumbwa blog yako ikashindwa kufanya vyema katika ulimwengu wa blog.

Blog ni nini?

Maana ya blog:

blog ni tovuti yenye maingizo yanayoitwa machapisho (posts) ambayo huonekana  katika kwa utaratibu wa kutangulia chapisho jipya kwanza na kufuatiwa na machapisho ya nyuma. Kwa mfano kama juzi, jana na leo umeandika machapisho na kuyachapa katika blog yako basi katika kurasa yako ya mbele litaonekana kwanza chapisho la leo kisha la jana na kisha la juzi. Blog huhusisha makala unazochapa (machapisho), viungo (links) na maoni  (comments) ya watembeleaji ili kuongeza maingiliano ya kimawasiliano kati ya blog na watembeleaji blog hiyo. Kwa kawaida blog huumbwa kwa programu maalum za kuchapishia.

Maswali 6 ya kujiuliza kabla hujaanzisha blog


maswali 6 ya kujiuliza kabla hujaanzisha blog“Je! unahitaji kuanzisha blog, kama ndio basi zingatia yafuatayo”
Kabla hujaanzisha blog na kutumia muda wako kuishughulikia ni vyema ukajitathimin mwenyewe katika mambo 6 yafuatayo;

Je! unapendelea kutumia muda wako mwingi katika mtandao wa intanet?
Kuanzisha blog, kuipromoti, na kuikuza ni kitu kinachohitaji mtu mwenye mapenzi ya kukaa katika komputa muda mwingi na kujisikia raha kwa huko kukaa kwake. Mwenye blog anahitaji muda kuandika post za blog yake, kupitia na kusoma blog za wenzake, kupitia post zake za nyuma na kuzihariri na kutafuta zana zitakazomsaidia kuifanya blog yake iwe bora zaidi. Hivyo basi kama huwa unajisikia tabu kukaa mbele ya kompyuta muda mwingi basi ni vyema ukatafuta ufumbuzi kabla ya kuanzisha blog.

Anzisha Blog

1) Je unahitaji kuanzisha blog yenye mafanikio?
2) Je wewe ni mwanablog mchanga na unahitaji kufahamu mengi yatakukufanya uwe ni mwenye mafanikio katika uwanda wa blog?
3) Je umeanzisha blog lakini unakata tamaa kwa kuwa huna muelekeo na hujui unachokifanya?
4) Je huamini kama unaweza ukaifanya blog yako ikatembelewa na watu zaidi ya elfu moja kwa siku?

Ikiwa angalau moja ya jibu katika majibu ya maswali hayo ni "ndio" basi umefika katika blog iliyosahihi kwa utatuzi wa tatizo lako. Fuatana nami katika mfululizo wa machapisho 10 muhimu ambayo nimeyaandaa mahususi kwa ajili ya wanablog wachanga ili waweze kujitambua wenyewe katika uwanda wa blog na kupata pa kuanzia.

Tupende katika Facebook

 
Msaada : All Tanzania Blogs Hakimiliki © 2013. All Tanzania Blogs
Blog Imebuniwa na Kuchapwa na: Tanzania Website Design Imewezeshwa na: Blogger