“Je!
Unaandika post lakini hazivutii wasomaji kuzisoma? Tazama mambo ya kuzingatia
ili itie mshawasha”
Wateja wa blog yako hawasomi post zako
kwa sababu tu zina ujumbe mzuri, la hasha! Ila pia kwa kuwa zinavutia machoni
na zinawafanya wajihisi wepesi kuanza kuzisoma. Kama post yako itakuwa ni
maneno tu yamejaa kurasa yote humfanya msomaji ahisi kuwa atachukua muda mrefu
kusoma na kuchanganua kilichoandikwa. Lakini kama itakuwa imepangiliwa vizuri
basi hatoona wingi wa maneno na ataanza kuelewa kinachozungumziwa kabla
hajamaliza kusoma.
Vifuatavyo ni vitu vitakavyomtamanisha msomaji asome post yako
1. Vichwa vya habari vya chapisho
Kazi iliyopangiliwa kwa kuwa na vichwa
vya habari vinavyotambulisha kila wazo katika post yako humfanya msomaji aelewe
anachokisoma baada tu ya kuona kichwa hicho. Mfano ukiandika post kisha baada
ya kichwa cha post yakajaa maelezo tu hadi mwisho itamlazimu msomaji aisome
kazi yote ndio apate picha ya kinachozungumziwa. Lakini kama baada ya kichwa
cha habari kikuu ukaandika aya moja kisha kikafata kichwa cha habari kidogo
kisha maelezo yake, kisha vivyo hivyo mpaka mwisho, kutamfanya msomaji aelewe
habari nzima kwa kusoma vichwa vya habari tu na hivyo huwa mwepesi kuisoma kazi
nzima.
2. Picha katika blog
Picha hutoa ujumbe kwa wepesi zaidi
kuliko maneno elfu moja. Matumizi ya picha hupunguza mlundikano wa maneno
pamoja na humpa msomaji kitu cha kujiburudisha akiwa katika post yako. Humfanya
msomaji apate ujumbe wa kinachozungumziwa na kukumbuka kwa wepesi zaidi ujumbe
ule. Picha inaweza ikawa ni ya kupiga kwa kamera, mchoro, chati ama jedwali. Ni
muhimu tu kuzingatia masuala ya haki miliki unapotumia picha.
3. Listi/orodha katika blog
Kutumia listi ni kujaribu kuyapanga
mawazo yako katika mtiriliko ambao utakuwa na vichwa vya habari na namba ama
nukta. Listi hufanya post ionekane nyepesi na yenye kusomeka. Jitahidi kutumia
listi katika post zako ambazo zinaruhusu listi. Post hii ni mfano mzuri wa
matumizi ya list.
4. Rangi za blog
Si kila post itakuwa na rangi yake, la
hasha! Ila mpangilio mzuri wa rangi katika post zako hupendezesha post na
kuonekana ni za maana hata kama yaliyomo hayafikii kiwango hicho cha umaana.
Jaribu kutumia rangi tofauti katika kichwa cha habari kikuu, vichwa vidogo,
linki na maneno yaliyobaki. Kwa kawaida kuseti rangi huwa kunafanyika wakati wa
kudizaini blog yako.
5. Video katika blog
Video zina faida kama ilivyo picha ila
kwa video ni zaidi. Kuna aina ya watu ambao huwa wanauwezo mkubwa wa kujifunza
kwa kusikia kuliko kusoma hivyo kwa video na sauti watavutiwa zaidi na blog
yako. Zipo tovuti ambazo unaweza kuweka video zako bure kisha ukaziunganisha
katika blog yako.
Post a Comment