Maana ya blog:
blog ni tovuti yenye maingizo yanayoitwa
machapisho (posts) ambayo huonekana katika kwa utaratibu wa kutangulia chapisho
jipya kwanza na kufuatiwa na machapisho ya nyuma. Kwa mfano kama juzi, jana na
leo umeandika machapisho na kuyachapa katika blog yako basi katika kurasa yako
ya mbele litaonekana kwanza chapisho la leo kisha la jana na kisha la juzi. Blog
huhusisha makala unazochapa (machapisho), viungo (links) na maoni (comments) ya watembeleaji ili kuongeza
maingiliano ya kimawasiliano kati ya blog na watembeleaji blog hiyo. Kwa
kawaida blog huumbwa kwa programu maalum za kuchapishia.
Program za kublog:
ü Blogger
(www.blogspot.com)
ü Wordpress
(www.wordpress.com)
ü Drupal
ü Movable
Type
ü TypePad
ü Livejournal
ü b2evolution
Mnyambuliko wa neno blog:
ü Kublog: kitendo cha kuandaa machapisho
na kuyachapa katika blog
ü Mwanablog: mtu ambaye anaandika machapisho
katika blog
ü Ulimwengu wa blogu: jumuiya/jamii/ ya wanablog
na vinavyohusiana na blog katika mtandao
Hali ya mtandao kabla ya kuanza kwa blog:
Kuanzia mwaka 1989 ulipogunduliwa mtandao
(Web 1.0) hadi 2004 mtandao ulikuwa ni kama chombo cha kutolea habari tu. Wenye
tovuti walikuwa wakitoa habari walizonazo lakini hapakuwa na nafasi ya
kumuwezesha mtembeleaji kuweza kutoa mchango wake katika habari hizo ama
kushiriki kwa namna yeyote zaidi ya kusoma na kutazama tu. Hivyo tunaita kuwa
mtandao ulikuwa ni wa mazungumzo ya upande mmoja tu na kuacha upande wa pili
kuwa wasikilizaji.
Baadae katika maendeleo ya mtandao kulianza
kuwa na maingiliano ambapo ulianzishwa utaratibu wa kuweza kununua kupitia
katika mtandao lakini bado mtandao ulibaki kuwa ni wa upande mmoja kutoa
taarifa na mwingine kusikiliza.
Mwaka 2004 wakati wa mageuzi “rasmi” ya
mtandao kutoka “Web 1.0” kuingia “Web 2.0” (mtandao wa kijamii) yalifanya maudhui
(contents) ya mtembeleaji kuwa ni sehemu muhimu ya ulimwengu wa mtandao. Leo
hii tuna mtandao ambao unajumuisha mazungumzo ya pande mbili ambapo mtembeleaji
anaweza kushiriki kwa kuingiza mchango wake kwa mtindo wa maoni na njia
nyinginezo za mitandao ya kijamii. Hapa ndipo blog ilipozaliwa katika ukamilifu
wake tulionao sasa (Ikumbukwe kuwa blog ilikuwepo tangu miaka ya 1990 lakini
hapakuwa na maingiliano na mtembeleaji)
Kuzaliwa kwa Blog:
Awali blog ilianza miaka ya 1990 kama
shajara (Diary) ya mtandaoni. Watu binafsi walikuwa wakichapisha habari na
matukio yao ya maisha ya kila siku na kutoa mitazamo yao juu ya mambo tofauti
wanayokutana nayo katika maisha. Machapisho yalikuwa yakijipanga katika blog
kwa kuanza na yale ya karibuni zaidi kisha kufuata na yaliyopita ili kuleta
maana zaidi kwa msomaji.
Kutokana na maendeleo ya mtandao viliongezwa
vitu vinavyowezesha kuwepo na mazungumzo ya pande mbili na kumfanya mtembeleaji
kuweza kutoa maoni yake ama kuongeza kiuno katika blog ama tovuti nyingine
kwenda katika blog aliyosoma ili kuongeza mjadala zaidi katika mtandao
Hali ya blog kwa sasa:
Mtandao uimekuwa zaidi wa kijamii, blogs zimepata
umaarufu mkubwa katika mtandao. Leo, kuna blog zaidi ya milioni 100 na kila
siku blog mpya zinaingia katika ulimwengu wa blog kila siku. Blog zimekuwa ni
zaidi ya shajara za mtandaoni. Kwa kweli, wanablog wamekuwa sehemu muhimu ya ulimwengu
wa mtandaoni na nje ya mtandao na wanablog maarufu wamekuwa wakileta athari
kubwa katika ulimwengu wa siasa, biashara na jamii kwa ujumla.
Mustakabali wa blog:
Ni suala lisilopingika kuwa wanablog
wanaonekana kuwa na nguvu zaidi katika siku zijazo na jamii na wafanya biashara
wametambua uwezo wao wa ushawishi katika kuvutia masoko na kubadili muelekeo wa
jambo katika jamii.
Kwa sasa kila mtu anaweza kuanzisha blog
bure kabisa ilimradi uweze kupata mtandao. Swali langu kwako ni je, unayo blog kwa
sasa? Kama unayo basi iweke katika kipengele cha maoni hapo chini. Kama hauna
basi tuambie kwa nini huoni umuhimu wa kuwa na blog yako.
+ maoni + 3 maoni
Natamani kuwe na Kiswahili cha blog. Napendekeza iitwe Kiingia Mtandaoni. Hapo tutapata kuwa kublog ni Kuingia Mtandaoni. Waonaje?
Ni vyema kuona blog za kiswahili zikishamiri, Kwa sasa Hali ya blog ni ya kuridhisha sana hapa Tanzania.
Topic Nzuri,
Hata mimi nimecover topic kama hii kupitia.
http://chapisha.com/blog-ni-nini/
Asante kwa kutuelimisha
Post a Comment