Sababu 5 kuu zinazowafanya watu wablog

all tanzania blogs
Kuna sababu nyingi zinazofanya watu waanzishe blog, lakini wengi wanaelezea kuwa wanablogu  kwa
sababu moja au zaidi kati ya sababu tano nitakazozielezea katika chapisho hili. Sababu hizi ndizo sababu kuu zinazowafanya wengi wa wanablog kuanzisha blog. Sababu hizi ni kwa wanablog wengi bila kujalisha aina ya mada anayoizungumzia iwe siasa, biashara, afya, elimu ama hata blog ya picha tu.

Kabla ya kuanzisha blog, tafakari ni sababu ipi inayokufanya utake kuwa mwanablog. Je malengo yako ya muda mrefu na mfupi ya kuwa mwanablog yanaendana na sababu inayokufanya uwe mwanablog? Hakikisha kuwa sababu inayokufanya kuwa mwanablog inaendana na malengo yako kinyume na hapo kuna uwezekano mkumbwa blog yako ikashindwa kufanya vyema katika ulimwengu wa blog.

1. Kublog kwa ajili ya burudani na kujifurahisha

Kuna idadi kubwa ya blogs zilizoanzishwa si kwa sababu nyingine ila kumfanya mwanablog kufurahi ama kufurahisha na kuburudisha watu wengine. Miongoni mwa blog zinazoingia katika kundi hili ni blog za vichekesho, blog zinazozungumzia wasanii maarufu, blog za michez, blog za sanaa, blog zinazotokana na vitu anavyopendelea mtu (hobby), baadhi ya blog za utalii na blog za picha. Nyingi za blog zinazozungumzia mada hizi huwa ni kwa ajili ya kujifurahisha na kufurahisha wengine. Pamoja na hayo pia zipo zinazozungumzia mada hizo lakini zimeanzishwa kwa sababu nyingine tofauti na hiyo.

Mifano ya blog hizo ni kama vile; chekavichekesho.wordpress.com, (kama unayo blog ya aina hii wasiliana nasi tuitaje hapa)

2. Kublog kwa ajili ya Netiweki na kujinadi

Baadhi ya watu huanzisha blog ili waweze kufahamika kuwa ni wenye utaalamu juu ya jambo fulani hivyo kupanua mitandao yao kwa kufahamiana na wataalamu wengine katika nyanja husika. Kupitia blogs zao, huweza kuonyesha utaalamu wao na kufikia watu wengi katika mtandao. Kupanuka kwa mitandao yao kutokana na maudhui ya blog yao kuwafikia watu wengi huweza kuwapatia fursa za kazi ama biashara.

Kwa mfano mhandisi wa nyumba mwenye kampuni yake binafsi anaweza kuanzisha blog inayozungumzia nyumba ama majengo ili aweze kuonyesha ujuzi wake na kujipatia fursa za biashara. Pia mpishi mkuu wa hoteli fulani anaweza kuanzisha blog inayozungumzia mapishi ili kukuonyesha ujuzi wake na kuweza kupata fursa ya kazi yenye maslahi mazuri zaidi naye. Hawa huweza kutimiza malengo yao kwa urahisi zaidi ikiwa wataunganisha jitihada zao za kublog pamoja na mitandao kama vile linkedin, twitter, google+ na facebook.

Mifano ya blog hizi ni kama vile: ... (kama unayo blog ya aina hii wasiliana nasi tuitaje hapa)

3. Kublog kwa ajili ya Biashara au uchochezi (Cause)

Baadhi ya blogu huanzishwa ili kuzipa nguvu bidhaa, biashara ama mashirika yasiyo ya faida. Maudhui ya blog yanaweza yasiitangaze bidhaa, biashara ama shirika moja kwa moja ila huweza ikawa imefungamana na tovuti, bidhaa, biashara ama shirika husika. Blog hizi huweza kutumika kutoa taarifa juu ya hizo bidhaa ama shirika na kuliwezesha shirika kupata mitazamo ya wateja wake kupitia blog hizo.
Blog nyingi zinazoingia katika kundi hili ni zile zinazoanzishwa na makampuni ama mashirika husika.

Mifano ya blog hizi ni kama vile: ... (kama unayo blog ya aina hii wasiliana nasi tuitaje hapa)

4. Kublog kwa ajili ya Uandishi wa Habari

Watu wengi huanzisha blog ili waweze kuwa kama waandishi wa habari wa raia. Wao huandika habari kuhusu matukio yanayotokea kila siku katika jamii yao ama hata kuhusu jamii ya kimataifa. Habari hizi huweza kuwa katika tasnia maalum kama vile siasa, michezo na uchumi ama huweza kuwa ni habari za jumla zinazojili kila siku. Blog zinazoanzishwa kwa sababu hii ndizo zimekuwa nyingi zaidi nchini Tanzania, na Kenya kuliko zinazoanzishwa kwa sababu nyingine.

Mifano ya blog hizi ni kama vile: ... (kama unayo blog ya aina hii wasiliana nasi tuitaje hapa)

5. Kublog kwa ajili ya Elimu

Baadhi ya watu huanzisha blog kwa ajili ya kuelimisha jamii juu ya mada fulani. Kwa mfano blog inayoelezea jinsi ya kuanzisha blog ama namna ya kutangaza blog yako hiyo ni blog inaweza ikawa ni miongoni mwa blog iliyoanzishwa kwa ajili ya kuelimisha.

Mifano ya blog hizi ni kama vile: ... (kama unayo blog ya aina hii wasiliana nasi tuitaje hapa)

Share this article :

Post a Comment

Tupende katika Facebook

 
Msaada : All Tanzania Blogs Hakimiliki © 2013. All Tanzania Blogs
Blog Imebuniwa na Kuchapwa na: Tanzania Website Design Imewezeshwa na: Blogger