Kabla hujaanzisha blog na kutumia muda wako kuishughulikia
ni vyema ukajitathimin mwenyewe katika mambo 6 yafuatayo;
Je! unapendelea kutumia muda wako mwingi katika mtandao
wa intanet?
Kuanzisha blog, kuipromoti, na kuikuza ni kitu kinachohitaji
mtu mwenye mapenzi ya kukaa katika komputa muda mwingi na kujisikia raha kwa
huko kukaa kwake. Mwenye blog anahitaji muda kuandika post za blog yake,
kupitia na kusoma blog za wenzake, kupitia post zake za nyuma na kuzihariri na
kutafuta zana zitakazomsaidia kuifanya blog yake iwe bora zaidi. Hivyo basi
kama huwa unajisikia tabu kukaa mbele ya kompyuta muda mwingi basi ni vyema
ukatafuta ufumbuzi kabla ya kuanzisha blog.
Je! Unapenda kuandika?
Kuwa na blog maana yake kuwa muandishi zaidi. Hata kama blog
yako itahusisha picha bado itahitaji utoe maelezo juu ya hizo picha, kujibu
koment/michango ya wateja wako, kuchangia katika blog za wengine na kadhalika.
Haya yote ni muhimu kwa mafanikio ya blog yako na ili yatimie basi unahitajika
uwe ni mwenye kupenda kuandika-andika tena mambo yenye maana.
Je! unaguswa na kuvutiwa na mada unayoiandikia?
Ili blog yako iwe na mafanikio unahitajika uwe post mara kwa
mara post zenye maana na zenye kuongeza kutu fulani kwa wasomaji wako. Hii
itasaidia kufanya upate wateja wapya na uweze kuwafanya wateja wako kuwa na
hamu na mahitaji ya kurudi tena katika blog yako. Ikiwa we mwenyewe hauguswi
sana na mada unayoiandikia basi hautaweza kuingia katika blog yako kila siku na
kuweka post mpya, ama unaweza kuweka post lakini si nzito katika uwanda
unaouandikia.
Je! Una msimamo?
Kama kweli unataka kuwa mwanablog basi ni lazima uwe na
msimamo na unachokifanya. Blog inataka uwe na ratiba ya kuishughulikia kila
siku. Inategemea na mada uliyochagua, utahitajika uende sehemu mbali mbali
kutafuta taarifa na habari zinazohusiana na blog yako, utahitajika usome vitabu
na mengineyo. Yote haya yatatumia muda wako mwingi lakini ni muhimu sana ili
blog yako iweze kuwa na post zenye kuwashawishi wateja wako kutembelea tena.
Je! Upo tayari na huuna hofu ya kutoa mawazo yako na
fikra zako kwa jamii?
Hebu fikiria hili, limetokea jambo katika jamii na wengi wa
waandishi, wanasiasa na wadau wengine katika uwanda wa jambo hilo wanasimamia upande
mmoja ambao wewe unaamini mtazamo huo si sahihi. Je unaweza kuthubutu kutoa
mawazo yako na kuonyesha upande unaosimamia pasi na hofu ya namna jamii
itakavyo kuchukulia? Mwanablog ni mwana mapinduzi na hapaswi kuwa na uoga wa
kutoa mawazo yake ambayo kwa upeo na uchanganuzi wake anayaona yanamanufaa
katika kuijenga jamii.
Je! Unaogopa kuwa haufahamu mengi kuhusu teknolojia ya
mtandao na haupo tayari kujifunza?
Mwanablog mwenye mafanikio hana hofu ya kuwa hajui jambo
fulani katika mitandao ya intanet. Anapogundua kuwa kuna kitu kipya katika
mtandao ambacho ni muhimu katika kuijenga na kuikuza blog yake basi hukitafuta,
hujifunza na kukifanyia kazi. Kuna vitu vingi vya kuvifahamu kama vile HTML,
SEO, CSS na mengineyo. Hata hivyo hayo si katika mambo ya msingi yanayohitajika
kukufanya ufanikiwe.
Post a Comment