Anzisha Blog

1) Je unahitaji kuanzisha blog yenye mafanikio?
2) Je wewe ni mwanablog mchanga na unahitaji kufahamu mengi yatakukufanya uwe ni mwenye mafanikio katika uwanda wa blog?
3) Je umeanzisha blog lakini unakata tamaa kwa kuwa huna muelekeo na hujui unachokifanya?
4) Je huamini kama unaweza ukaifanya blog yako ikatembelewa na watu zaidi ya elfu moja kwa siku?

Ikiwa angalau moja ya jibu katika majibu ya maswali hayo ni "ndio" basi umefika katika blog iliyosahihi kwa utatuzi wa tatizo lako. Fuatana nami katika mfululizo wa machapisho 10 muhimu ambayo nimeyaandaa mahususi kwa ajili ya wanablog wachanga ili waweze kujitambua wenyewe katika uwanda wa blog na kupata pa kuanzia.

Kabla hujaanza hata kufungua blog yako nakushauri kitaalamu kuwa upitie machapisho 10 yafuatayo kwa umakini na kuelewa ili uwe ni mwenye mwanzo mzuri wa blog yako/zako. Hata kama ulikwishaanza lakini unahisi hufanyi vyema basi pia tenga muda wako kwa siku na taratibu pitia machapisho yafuatayo ili utambue ni wapi umekosea ama ni wapi panahitaji kuongezea ama ni kitu gani cha kupunguza ili blog yako iwe ni ya mafanikio.

Machapisho blog yenyewe ni:

02) Sababu 5 kubwa za watu kublog
03) Sababu 10 zinazoweza kukufanya uanzishe blog
04) Angalia kama kublog kunakufaa kabla hujaanza
05) Jipime kama unastaili kuanzisha blog
06) Tambua vitu 5 unavyoweza kuchukia katika kublog kwako
07) Mahitaji muhimu ili uanzishe blog yenye mafanikio
08) Vidokezo 10 vya kuzingatia kwa wanablog wachanga
09) Vidokezo vya kublog muhimu kwa kila mwanablog
10) Vidokezo 5 katika kuchagua mada kwa ajili ya blog yako

Usisite kuuliza swali sehemu yeyote ambayo utakuwa unahitaji ufafanuzi katika chapisho husika. Na kama utaona machapisho haya yanamanufaa basi pia unaweza kushirikisha (share) na wenzio kwa kutumia viungo vilivyopo chini ya hili chapisho.
Share this article :

Post a Comment

Tupende katika Facebook

 
Msaada : All Tanzania Blogs Hakimiliki © 2013. All Tanzania Blogs
Blog Imebuniwa na Kuchapwa na: Tanzania Website Design Imewezeshwa na: Blogger